TAMISEMI inapenda kuutarifu Umma kuwa, baada ya uhakiki wa
uripoti wa walimu walioajiriwa Mwezi Desemba, 2017, jumla ya Walimu
45 (walimu 20 wa Shule za Msingi na 25 wa Shule za Sekondari)
hawakuripoti kwenye vituo walivyopangiwa. Hivyo, OR-TAMISEMI
imewapangia walimu wengine ili kujaza nafasi wazi za walimu hao katika
Shule kwenye Halmashauri ambazo hawakuripoti. Walimu hao
wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vya kazi ndani ya siku 14 kuanzia
tarehe 17/03/2017.
Wakurugenzi wa Halmashauri wanaelekezwa kuwapokea Walimu hao na
kukamilisha taratibu za ajira kwa kuzingatia taratibu na kanuni za
utumishi wa Umma, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya kuripoti kwao.
Taarifa ya kuripoti waajiriwa hao itumwe Ofisi ya Rais - TAMISEMI
ifikapo au kabla ya tarehe 02.04.2017.
Majina ya Walimu hao waliopangiwa vituo yanapatikana katika tovuti ya
Ofisi ya Rais - TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
To see the names of Primary School Teachers please CLICK HERE
To see the names of Secondary School Teachers please CLICK HERE
Source: TAMISEMI Official Website
No comments:
Post a Comment